Ijumaa 6 Februari 2026 - 06:00
Kutunukiwa kwa Tuzo ya Benki ya Kiislamu ya mwaka 2026 kwa mwanazuoni wa Kishia

Hawza/ Kwa kuthamini miaka mingi ya huduma zenye athari katika maendeleo ya benki na fedha za Kiislamu, Tuzo ya Benki ya Kiislamu ya mwaka 2026 imetolewa kwa Hujjatul-Islam wal-Muslimin Shabbir Hasan Meethami katika hafla rasmi iliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Minhaj, Lahore, Pakistan.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, tuzo hiyo ilitolewa kwa Hujjatul-Islam wal-Muslimin Shabbir Hasan Meethami, mshauri wa zamani wa kisheria wa Benki Kuu ya Pakistan, rais wa “Taasisi ya Al-Sadiq kwa Fedha za Kiislamu na Takaful”, na katibu mkuu wa Baraza Kuu la Wanazuoni wa Kishia nchini Pakistan; shakhsia iliyokuwa na mchango mkubwa katika kuimarisha misingi ya fedha za Kiislamu na kuboresha mifumo ya kifikh katika mfumo wa benki wa nchi hiyo.

Sherehe ya utoaji wa tuzo hiyo ilifanyika wakati wa Mkutano wa Kimataifa wa Tisa wa Uchumi na Fedha za Kiislamu, katika hafla kubwa iliyoandaliwa katika Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Minhaj mjini Lahore, Pakistan. Katika hafla hiyo, Dkt. Hussein Mohiuddin Qadri, mjumbe wa bodi ya uongozi na naibu wa chuo hicho, alimkabidhi Hujjatul-Islam wal-Muslimin Shabbir Hasan Meethami cheti cha heshima na tuzo ya benki ya Kiislamu.

Katika kongamano hilo la kielimu, viongozi na wataalamu mashuhuri wa sekta ya fedha za Kiislamu walihudhuria, wakiwemo wataalamu na wachambuzi wa tasnia ya fedha za Kiislamu kutoka nchi mbalimbali kama Algeria, Iran, Australia, Bahrain, Brunei, Bangladesh, Uturuki, Malaysia, Singapore na nchi nyingine. Washiriki hao walipongeza mchango muhimu wa Hujjatul-Islam wal-Muslimin Shabbir Hasan Meethami katika kuendeleza na kueneza benki ya Kiislamu katika ngazi ya kitaifa na kimataifa.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha